Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwa Mkoani Njombe Januari 30, 2021 amesema kuwa, Serikali imeanza maandalizi ya ujenzi wa miradi miwili mikubwa ya kufua umeme wa jumla ya megawati 580 kwa njia ya maji ambayo ni, Mradi wa Ruhudji na Mradi wa Rumakali yote kwa pamoja ikiwa Mkoani Njombe.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani Desemba 14, 2020 akiwa katika ziara ya kukagua ujenzi wa Mradi mkubwa wa kufua umeme wa Megawati 2115 kwa njia ya maji wa Julius Nyerere, amesema inatarajiwa kwa mwaka 2023 mahitaji ya umeme Nchini yakaongezeka kwa zaidi ya mara mbili mpaka kufikia megawati 2,770
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeingia mkataba wa kununua umeme kutoka kwa wazalishaji wadogo wa kampuni sita binafsi, utakaoingia moja kwa moja kwenye kwenye gridi ya Taifa na kutumika katika maeneo mbalimbali Nchini.