Bei ya umeme inatofautiana kutokana na kundi la matumizi mteja alilopo mfano Matumizi Madogo ya nyumbani (D1) ambao wanatumia umeme wa majumbani ambao matumizi yao ni wastani wa KWh 75 kwa mwezi wananunua umeme uniti moja kwa Tsh 100 (bila kodi) endapo watazidi hapo kila unit watatozwa Tsh 350 (bila kodi), Lakini wateja wa kundi la matumizi ya kawaida (T1) Kundi hili hujumuisha wateja wenye matumizi ya kawaida ya umeme hususani watumiaji majumbani, biashara na viwanda vidogo, taa za barabarani na mabango -  wananunua umeme Unit moja Tsh 292 (bila kodi), kundi hili linatumia kuazia unit 75-7500 kwa mwezi. Hivyo kutofautiana kwa kundi la matumizi ndicho kinachopelekea wateja kupata unit tofauti kwa kiasi kilekile cha pesa.