Shirika la Umeme TANESCO limesema kuwa Uhakika wa umeme unaonekana sasa kwa mikoa iliyoungwa kwenye grid ya taifa unatokana na kuendelea kuwashwa kwa mitambo ya kufua umeme kwa kutumia gesi. Mitambo hiyo ni ya Kinyerezi 150 MW, Ubungo 2 (105MW) na Symbion 112 MW. Mvua zilizoanza kunyesha bado hazinyeshi kwenye  mikoa yenye mito inayoweza kujaza Bwawa la Mtera, Kidatu na Kihansi ambayo ndio vyanzo vikubwa vya kufua umeme wa maji. Hayo yalisemwa leo na Meneja Uhusiano TANESCO Adrian Severin wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Ubungo jijini Dar es salaam.


"Tanesco imejipanga kuwahudumia watanzania.  Hali ya Umeme nchini imeimarika sana kwa sasa kutokana na ujao wa gesi, na bado kuna mitambo inaendelea kuwashwa. Mtuamini. Alisema Severin.