TANESCO MDSHIRIKA la Umeme Nchini Tanzania, (TANESCO), limesaini mkataba na makampuni matatu kujenga njia ya umeme, (Transmission lines), ya Msongo wa Kilovolti 400 Tanzania na utakaounganisha Kenya.

Hafla ya kutiliana saini mikataba hiyo, imefanyika Oktoba 7, 2016 Makao Makuu ya TANESCO Jijini Dar es Salaam, ambapo TANESCO Shirika, imetiliana saini mikataba hiyo na makampuni ya Bouygues Energies Service, Energoinvest na Kalpa-Taru.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi, Felchesmi Mramba, alisema, Ujenzi wa Mradi huu wenye urefu wa Kilomita 414, utaanzia Mkoani Singida,-Babati-Arusha hadi Namanga kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya.

Kisha Mradi utaunganishwa na njia ya Msongo wa Kilovolti 400 yenye urefu wa kilomita 96 kutoka eneo la Isinya, Nairobi, nchini Kenya hadi eneo la mpaka wa Tanzania na Kenya, (Namanga) ambapo utaunganisha na njia ya umeme wa wa Msongo wa Kilovolti 400kv kwa upande wa Tanzania.

“ Napenda niwahakikishie, kuwa huu ni mfululizo wa miradi mikubwa inayotekelezwa na TANESCO na utawezesha usafirishaji wa umeme wa Mgawati 2000 katika pande zotekenya na Tanzania”. Alifafanua Mhandisi Mramba. Akifafanua zaidi, Mhandisi Mramba alsiema, utekelezaji wa mradi huu unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB), na Shirika la Misaada ya Maendeleo la Japan, (JICA), kwa gharama ya Dola za Kimarekani, Milioni 309.26 utakamilika katika kipindi cha miezi 24, sawa na miaka 2. “Dola za Marekani Milioni 258.82, zitatumika kujenga upande wa Tanzania na  Dola za Kimarekani Milioni 50.45 zitatumika kujenga mradi upande wa Kenya,” alifafanua Mhandisi Mramba.

Aidha Mhandisi Mramba aliwataka wakandarasi waliopewa kazi hiyo kuitekeleza kwa wakati kwa mujibu wa mkataba.

“ Agizo, kwenu ninyi wakandarasi, kamilishini mradi ndani ya muda kama ambavyo tumekubaliana kwenye mkataba, kushindwa kukamilisha ujenzi kwa mujibu wa mkataba ni kushindwa kufanya kazi na sisi kama TANESCO hatutakubaliana na hilo.” Alionya Mhandisi Mramba.

Naye mwakilishi Mkazi wa (AfDB), Tonia Kandiero, alitoa hakikisho kuwa benki hiyo itaendelea kusaidia miradi mikubwa kama hii, kwa manufaa ya eneo lote la Afrika.
Kwa upande wake, MAfisa Miradi msaidizi wa JICA, Apolei Rosina, naye aliungana na AfDB, kutoa hakikisho la ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na JICA, katika kusaidia kutekeleza miradi ya maendeleo kama huu uliosainiwa.

Images of the event