Untitled5WAHANDISI 12 kutoka Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), wamemaliza mafunzo ya wiki mbili katika Sekta ya Nishati na Umeme yaliyofanyika kwenye Nchi za Italia na Hungary.

Mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Mkurugenzi wa Pietro Fiorentini Tanzania Bw. Abdulsamad Abdulrahim yalihusisha Mameneja Waandamizi na wafanyakazi wengine wa TANESCO kwa nia ya kujenga uwezo wa kiutendaji katika sekta hizo na yamefungwa Aprili 7, 2017.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Pietro Fiorentini hapa nchini, Bw. Abdulsamad Abdulrahim imesema, Wahandisi hao 12 wa TANESCO walijifunza masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na mpango wa ufundi(Technical design), Uhandisi, (Engineering), uunganishaji, (Asembling), uendeshaji, (Operations), Afya, (Health), Usalama(Safety), matengenezo, (Maintenance) na ufundi, (Troubleshooting).

Baada ya mafunzo hayo, washiriki walipatiwa vyeti vya ushiriki lakini pia walipata fursa kwa mara ya kwanza kushiriki kwenye utafiti wa maendeleo (Research & Development), ambapo walijionea ya vifaa vipya huku wakiangalia wahandisi waliopewa jukumu la kutumia utafiti katika eneo la teknolojia huku mbeleni.

Aidha Bw. Abdulrahim amesema, washiriki wamesema mafunzo hayo yamekuwa na manufaa makubwa kwao na yataongeza thamani katika utendaji kazi wao na kuiomba Pietro Fiorentini kuwapatia nafasi zaidi wahandisi wa TANESCO ili kuwajengea uwezo zaidi kama wao