Naibu Waziri awasha kituo cha MbagalaNaibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu Februari 22, 2018 amewasha Kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Mbagala chenye uwezo wa 50 MVA na hivyo kuimarisha upatikanaji wa umeme katika baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam. Akizungumza jijini Dar s Salaam, Mhe. Mgalu alisema kuwashwa kwa Kituo hicho kutaondoa changamoto ya umeme iliyokuwa ikiyakabali maeneo ya Mbagala, Kigamboni, Mkuranga, Tandika na Kurasini, Maeneo hayo yatapata umeme wa uhakika.

Aliongeza kituo cha Mbagala kilikuwa kimezidiwa kutokana na mahitaji makubwa ya umeme katika maeneo hayo, kutokana na mitambo kuwa chakavu. “Niwashukuru Bodi ya TANESCO kwa kusimamia hili vizuri, Menejimenti pamoja na Watendaji wa TANESCO kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuboresha miundombinu ya umeme”. Alisema Mhe. Mgalu.’

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO Dkt. Alexander Kyaruzi aliwataka Wananchi wa Mbagala kuchangamkia fursa hiyo, kwani umeme wa uhakika sasa utapatikana katika maeneo hayo. “Ndani ya siku tatu Wananchi wa Mbagala wataanza kuona tofauti, hii ni kutokana na kuwashwa kwa Kitu”. Alisema Dkt. Kyaruzi.