WebsiteWaziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani ameongoza ujumbe wa Tanzania Nchini Morocco kwa mwaliko wa Waziri wa Madini na Maendeleo ya Nishati   wa Morocco katika Mkutano wenye lengo la kukuza ushirikiano katika sekta za Nishati na sekta ya madini baina ya nchi hizi mbili.

Katika Ziara yake nchini Tanzania  mnamo 2016 Mfalme wa Morocco pamoja na mambo mengine aliainisha nia ya nchi yake kukuza ushirikiano na Tanzania hususan katika sekta ya Nishati ambapo pia alisaini makubaliano ya awali(MOU) kati ya Wizara ya Nishati ya Nchini Morocco na iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini ya Tanzania.

Katika ziara hiyo Wizara ya Madini iliwakilishwa na Katibu Mkuu Prof. Msanjila na Kamishna wa Madini bw. David Mlabwa.

Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani katika ziara hiyo, ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPDC Mhandisi Kapuulya Msomba pamoja na wataalamu wengine wa Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini.