Utekelezaji mradi ZTKMRADI wa Umeme wa Kenya-Tanzania Power Interconnection (KTIPIP) ZTK tayari umeanza kutekelezwa ambapo kazi ya kutengeneza misingi ya kusimika minara (towers) imeanza.

Mratibu wa Mradi huo Mhandisi Peter Kigadye aliwaambia Wahariri wa Vyombo vya Habari waliotembelea kambi ya Wakandarasi iliyoko Kijiji cha Nanja kilichoko barabara ya Bababti-Arusha Wilayani Munduli Januari 22, 2019.

Mradi huo ni sehemu moja ya mradi mzima wa Regional Power Connection ambao lengo lake ni kuunganisha Mfumo wa Umeme wa Tanzania na Afrika Mashariki (East Africa Power Pool) kwa upande wa Kaskazini, na baadaye utekelezaji wa sehemu nyingine ya tatu ambayo itakuwa inaunganisha mifumo ya nchi Kusini mwa Afrika, kupitia chombo kinachoitwa Southern Africa Power Pool (SAPP)

 “Tanzaania tumebarikiwa tutakuwa na sehemu tatu, sehemu ya kwanza ni mradi wa Backborn ambao umejengwa katikati ya nchi yetu, ulikuwa na kilometa 670 ambao unaanzia Iringa hadi Shinyanga, sehemu ya pili ni kuunga kutoka Singida hadi mpakani na Kenya kuna kituo kimoja kinaitwa Isinya, jumla hapo kuna kilometa 510.7 na hizo ndio kilomita za mradi tunazoanza kuutekeleza hivi sasa.” Alisema Mhandisi Kigadye. 

Aliongeza kuwa sehemu ya tatu ni kuanzia Iringa kwenda Kusini ambapo kuna mradi utakaoitwa Zambia Interconector ambao una kilometa 624 na kusema Tanzania itakuwa imekamilisha msongo wa kilovoti 400

Aidha, Mhandisi Kigadye alisema kuhusu kuunganiushwa kwa umeme kwenye nchi za Ukanda wa Mashariki na Kusini lengo ni kuunganisha nchi yetu na nchi za Kikanda kuanzia Kaskazini kuungana na Kenya na Kusini kuungana na Zambia.

Alisema mradi wa Kenya-Tanzania Power Interconnection (KTIPIP)ZTK, utakamilika Aprili 2020, wakati ule Zambia Connector unatarajiwa kukamilika utakamilika mwaka 2022.

"Tutakuwa tumemaliza mikongo hii mitatu (3)na nchi yetu itakuwa tayari kushiriki kwenye biashara ya umeme Kikanda", aliongeza Mhandisi Kigadye.

Akifafanua zaidi kuhusu mradi huo wa Kenya-Tanzania Power Interconnection (KTIPIP)ZTK alisema sehemu ya kwanza itahusu ujenzi wa njia za kusafirisha umeme (transmission lines) na ujenzi wa vituo vya kupozea umeme.

Mradi mzima una urefu wa kilometa 510 na umegawanyika kwenye sehemu nne, ambazo ni Isinya Kenya hadi Namanga Kilometa kilomita 96, sehemu ya pili unahusu Namanga - Arusha Kilometa 114, sehemu ya tatu Arusha-Babati kilometa 150, na Bababti-Singida kilometa 150.

Kwa upande wake,  Mhandisi Emmanuel Manirabona ambaye ni Meneja Mwandamizi Miradi, alisema tayari vifaa vya kutekeleza ujenzi wa mradi huo vimewasili kwa kiasi kikubwa cha kazi imeshaanza.

Akieleza zaidi Mhandisi Manirabona alibainisha kuwa kila kitu kiko sawa na Wananchi wote ambao wako kwenye sehemu mradi unakopita, tayari Serikali imeshawalipa fidia na ndiyo maana Mkandarasi anaendelea na kazi.