Power 2 WebsiteTaifa lolote linalotamani kuwa na maendeleo endelevu, ni lazima lihakikishe nishati ya umeme inapatikana kwa uhakika kwani ndiyo mhimili muhimu wa maendeleo na ukuaji wa uchumi.


Ndiyo maana mataifa yote yaliyoendelea dunia yamewekeza vizuri katika sekta ya umeme wakiamini ndiyo kichocheo katika kukuza uchumi imara.
Kwa lugha nyingine ni kuwa kama nchi haina umeme wa uhakika, ni vigumu kufikia malengo tuliyojiwekea kimataifa na kitaifa.


Ni kwa kutambua hilo, Serikali ya Awamu ya Tano imejikita zaidi kuwekeza kwenye miradi ya kimkakati ya kufua na kusambaza huduma ya umeme.
Hivyo, ili kuendana na kasi ya ukuaji uchumi na ongezeko la mahitaji kwa Taifa, Serikali kupitia TANESCO imeendelea kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati itakayoongeza ufuaji wa umeme.


Kama ilivyo azma ya Serikali ya kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati ifikapo 2023, tutafika huko tukiwa na umeme wa kutosha, uhakika, wa gharama nafuu katika kufua na kuuza na unaotabirika.


Aidha, ili kufua umeme kwa gharama nafuu Serikali imedhamilia kuachana na matumizi ya mafuta mazito ifikapo Agosti mwaka 2020.
Umeme unaotokana na matumizi ya mafuta umekuwa ukiigharim Serikali fedha nyingi.


Hili litafanikiwa kwa kuunganisha nchi nzima na mtandao wa gridi ya Taifa, hadi sasa Mikoa miwili ya Kigoma na Katavi ndio haijafikiwa na mtandao wa gridi.
Mipango madhubuti ipo kuhakikisha gridi ya Taifa inafika kwenye Mikoa hiyo, tayari ujenzi wa miundombinu mikubwa ya kusafirisha umeme wa kilovolti 132 imeanza tangu Desemba mwaka 2018 kutoka Tabora kupita Urambo kwenda mpaka Nguruka hadi Kidahwe Kigoma mjini kilomita 411.


Eneo la pili la ujenzi ni kutoka Tabora kupitia Ipole kwenda Inyonga hadi Nsimbo Mkoani Katavi umbali wa kilomita 371 ambako nako taratibu za ujenzi zimeanza na inatarajiwa kufikia Agosti 2020 Mkoa wa Katavi nao utakuwa umeunganishwa na gridi ya Taifa.


Hivi karibuni Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akiwa katika kikao na Bodi ya Wakurugenzi TANESCO, pamoja na Menejimenti, alisema malengo na dira ya Taifa ni kufikia megawati 5000 hapo 2020 na megawati 10,000 ifikapo 2025.


Dkt. Kalemani aliitaka Bodi na Menejimenti kusimamia na kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati.
Kwa kuangalia muktatha huo tunaona kabisa nia ya Serikali ni kuwafikia Wananchi wengi zaidi mijini na vijijini lakini pia uwepo wa umeme wa kutosha utakao saidia kuendesha viwanda.


Kuhusu suala la umeme Vijijini, Serikali imedhamiria kuvifikishia huduma ya umeme vijiji vyote nchini ifikapo 2021 kwa gharama ya Shilingi 27,000/= tu.
Miradi yote ya umeme vijijini inatekelezwa kwa gharama nafuu ili kuwawezesha Watanzania wengi zaidi wananchi wengi zaidi waweze kumudu kuunganisha huduma hii muhimu kwa maendeleo ya Taifa.


TANESCO pia imejikita katika uwekezaji wa utoaji wa huduma ya uhakika kwa maendeleo endelevu, lakini pia kwa kuwasogezea wananchi huduma karibu.
Katika kuboresha utoaji wa huduma kwa Wateja, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linaendelea na utaratibu wa kuwafuata Wateja maeneo mbali mbali nchini hasa wa Vijijini.


Wananchi walikuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma jambo ambalo lilikuwa likiwakatisha lilikuwa tamaa kuunganisha hudumaya umeme.