Website Rusumo kukamilikaUtekelezaji wa Mradi wa kufua umeme kwa maji unaotekelezwa kwa ushirikiano wa nchi tatu za Tanzania, Rwanda na Burundi Rusumo Hydropower umekamilika kwa asilimia 47.

Mradi huo unatarajiwa kufua megawati zipatazo 80 ambapo kila nchi itapata megawati 27.

Akifafanua baada ya kukamilika kwa kikao kilicho jumuisha Mawaziri wa naoshughulikia Nishati ya umeme kutoka nchi hizo, Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alisema hii ni mara ya tatu kwa Mawaziri kukutana kwa ajili ya kufuatilia hatua za utekelezaji.

Aliongeza, utekelezaji wa mradi upo kwenye hatua nzuri na unatarajiwa kukamilika kwa wakati Februari 2020.

Mradi wa Kufua Umeme kwa njia ya maji Rusumo Hydropower, unafadhiliwa na Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Serikali za Tanzania, Rwanda na Burundi.