Mwinuka press Janu 2020Sekta ndogo ya Nishati ya Umeme kupitia TANESCO imekuwa na mafaniko kwa kipindi cha miaka 4 katika Ufuaji wa umeme, Uzalishaji, Usambazaji na Uwekezaji.

Akiongelea mafanikio katika Sekta ndogo ya Nishati ya Umeme Nchini kwa kipindi cha miaka 4 ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Magufuli, Mkurugenzi Mtendaji TANESCO Dkt. Tito Mwinuka alisema katika kipindi hicho Serikali kupitia TANESCO imeongeza kwenye gridi ya taifa takribani Megawati 400 kutoka vituo vilivyoanza uazlishaji wa umeme kwa ktumia gesi asilia.

Alivitaja vituo hivyo ni Kinyerezi I Megawati 150, kilikamilika mwezi Machi 2016 kwa gharama ya silingi Bilioni 419 zote zikiwa ni fedha za ndani.

Miradi mingine ni Kinyerezi II Megawati 248, ulikamilika mwezi Septemba,2018  kwa gharama ya shilingi Bilioni 790 na mradi huu unamilikiwa na serikali kwa asilimia 100, pamoja na uboreshaji upatikanaji wa umeme katika Mikoa ya Lindi na Mtwara TANESCO ilitumia fedha za  ndani kununua mitambo 2 yenye uwezo wa kuzalisha Megawati 4 ili kuboresha upatikanaji wa nishati ya umeme katika Mikoa hiyo.

Kwa upande wa Njia Kuu za Kusafirisha umeme Dkt. Mwinuka  aliielezea miradi ambayo imeshakamilika ni mradi wa kutoka Iringa hadi Shinyanga kupitia Mikoa ya Dodoma na Singida (400kV)umbali wa kilometa 670 ambao ulikamilika mwezi Desemba, 2016 kwa gharama ya shilingi Bilioni 512, unamilikiwa na serikali kwa asilimia 100.

Mradi wa kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 220(220kV) kutoka Makambako hadi Songea wenye urefu wa Kilomita 250 kwa gharama yaa shilingi Bilioni 216 zikiwa fedha za ndani, ulikamilika rasmi mwezi Septemba, 2018.

Aidha, kwa kutumia pesa zake za ndani TANESCO imefanikiwa kujenga njia ya kusafirisha umeme  wa msongo wa kilovolti 132 urefu wa kilomita 80 kutoka Mtwara hadi Mahumbika kwa gharama ya shilingi Bilioni 15.

Aliongeza kuwa, katika kuboresha hali ya usafirishaji umeme katika jiji la Dar es salaam TANESCO imefanikiwa kukamilisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 132 kutoka Ubungo - Kipawa - Gongo la Mboto - Mbagala - Kurasini  na vituo vyake ya kupoza umeme.

Dkt. Mwinuka akifafanua zaidi alisema TANESCO imefanikiwa kukamilisha mradi wa ufungaji wa Transfoma ya Ukubwa wa Megawati 240 katika kituo cha kupoza umeme cha Ubungo, mradi ambao unatoa fursa  kwa Shirika kuweza kufanya matengenezo ya baadhi ya vituo vya kuzalisha umeme ambavyo vinazalisha katika msongo wa kilovoti 132 bila kuathiri hali ya upatikanaji umeme katika jiji la Dar es salaam, Pwani na Zanzibar.

Kuanzia mwaka 2016/2017 TANESCO ilianza kujiendesha bila kupata ruzuku kutoka Serikalini hii ni kutokana na Shirika  kuachana na mitambo ya kuzalisha umeme kwa gharama kubwa

Kuzimwa kwa vituo vya kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta Vituo hivyo ni Liwale, Tunduru, Namtumbo, Songea, Madaba, Mbinga, Ludewa na Ngara, ambapo takribani hilingi Bilioni 23.5 zinaokolewa kila mwaka baada ya Serikali  kuzima mitambo hiyo.

Akizungumzia miradi ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa na inayotarajiwa,  Dkt. Mwinuka alisema kuwa ni pamoja na mradi wa Kufua umeme kwa maji wa Julius Nyerere Megawati 2115 unaotekelezwa na Serikali kwa gharama ya shilingi trilioni 6.55, Rusumo Megawati 80, Kakono Megawati 87 na Mradi wa kuzalisha umeme kwa gesi Mkoani Mtwara megawati 300.

Akieleza zaidi, Dkt. Mwinuka alisema kuwa miradi mingine inatekelezwa katika maeneo mengine kwenye Mikoa mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na huduma ya umeme.