Ziara ya Kamati Kinyerezi I 2020Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imefanya ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi wa Kinyerezi I Extension.

Akiongea katika ziara hiyo, Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alisema lengo lingine la ziara ya Kamati ni kujionea miundombinu ya kufua umeme.

Alisema mradi wa Kinyerezi I Extension unahatua tatu ambazo ni upanuzi wa kituo, kuunganisha mradi wa Kinyerezi I na Kinyerezi I Extention pamoja na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme Gongo la Mboto.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge Mhe. Dustan Kitandula alisema Kamati imefika kuona hatua za uendelezaji wa mradi baada ya Mkandarasi wa kwanza kushindwa kuendelea na kazi na kujiridhisha iwapo hakuna mgogoro wa kimkataba.

“Mkandarasi wakati anafanya kazi alitoa kazi kwa kampuni za kitanzania, tumeitaka Serikali kuzilipa kampuni hizo za ndani ili waendelee na biashara zao”, alisema Mhe. Kitandula.

 Aliongeza Kamati imeridhishwa na mchakato unaoendelea wa kumpata Mkandarasi mwingine atakaye malizia kazi iliyobakia.

 Aidha asilimia 84 ya mradi imekamilika imekamilika na mradi unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka huu.

Eneo la Kinyerezi linamiradi mikubwa minne ambayo ni mradi wa Kinyerezi I, Kinyerezi II, Kinyerezi I Extension ambao upo katika hatua ya utekelezaji.

Miradi mingine ni Kinyerezi III ambao upo kwenye upembuzi yakinifu na Kinyerezi IV.

Vituo vya Kuzalisha Umeme vya Kuzalisha Umeme kwa kutumia gesi vinachangia megawati 892 kwenye gridi ya Taifa ambayo ni sawa na asilimia 51.54.