Ziara ya Bodi Pangani Nov 2020Bodi ya Wakurugenzi TANESCO ikiongonzwa na Mwenyekiti wa Bodi Dkt. Alexander Kyaruzi imeridhishwa na utendaji kazi wa kituo cha kufua umeme cha Pangani chenye uwezo wa Mw 68.

Katika kituo hicho cha Pangani Bodi ilikagua mitambo ya kuzalisha umeme na kuridhishwa na utendaji kazi kituoni hapo. Pia bodi ilipata fursa ya kutembelea mtambo wa kuingizia maji ambayo pia yanakwenda kufua umeme kituo cha ya Hale.

Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO ipo katika ziara ya siku sita kutembelea na kukagua shughuli mbalimbali za TANESCO katika Mikoa ya Pwani, Tanga, Kilimanjaro na Manyara.