FREQUENTLY ASKED QUESTIONS

#TitleDescription
1Je nikifichua mwizi wa umeme napewa zawadi?

Inategemea, endapo taarifa mteja aliyotoa itapelekea kukamatwa kwa mtuhumiwa na kudhihirika kuwa anaiba umeme, shirika litafanya hesabu na kubainisha kiasi cha hasara iliyopatikana, kutokona na kiasi hicho kilichookolewa mteja atapatiwa zawadi baada ya kufanyika kwa hesabu.

2Mwenye nyumba yangu anatutoza bei ya umeme kubwa zaidi kuliko TANESCO, nifanye nini?

Wateja wanapaswa kulipa bei ile ile ambayo shirika linatoza,hakuna anaruhusiwa kuuza umeme bila kibali cha mamlaka zinazohusika.Aidha wateja wanashauriwa kuhakikisha maswala yote ya malipo ya umeme au endapo kutakuwa na deni yanaingizwe kwenye mkataba wa pango ili kuondoa sitofahamu ambayo inaweza kujitokeza baadaye.

3Nataka kufunga mita ya pili kwenye nyumba yangu ili nijitenganishe na wapangaji, nifanye nini?

Hakikisha mita ya kwanza haina deni au haikuchezewa. Fika ofisi za TANESCO na kitambulisho utapatiwa fomu hakikisha unakuja na namba ya mita ya mwanzo. Baada ya hapo hatua zote ambazo mteja amezipitia kuomba umeme awali zitafuatwa kama ambavyo tumeonyesha kwenye sehemu ya taratibu za kufuata ili kufungiwa umeme.

4Natumia mita ya remote/King’amuzi kuna mpangaji ameondoka au ameharibu king’amuzi, nifanye nini?

Jina halisi ni CIU na sio king’amuzi au remote,mteja anayeibiwa au kupoteza CIU anapaswa kutoa taarifa kituo cha polisi ili kupatiwa loss report (Taarifa ya kuonyesha kuibiwa) kisha ataaandika barua kwenda kwa meneja wa Mkoa husika huku akiambatanisha taarifa ya polisi (loss report) mara baada ya wataalamu wetu kujiridhisha  mteja ataruhusiwa kulipia kiasi cha  Tsh 70,800.00 kama ni cha njia moja (Single moja) au Tsh 236,000.00 kama ni cha njia tatu (Three phase).