Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameikabidhi TANESCO tuzo iliyotolewa na TANTRADE ya utoaji wa huduma bora na ya haraka (appreciation award), iliyowezesha maandalizi mazuri ya Maonesho ya 48 ya kibiashara ya kimataifa Dar es Salaam (sabasaba).
TANESCO imepokelewa tuzo hiyo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dkt. James Mataragio katika ufunguzi wa maonesho hayo uliofanyika tarehe 3 Julai 2024 ambapo Mhe. Rais Samia alikua mgeni rasmi akiambatana na Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi.