
Akikagua ujenzi wa kituo cha kupokea, kupoza na kusambaza umeme Mpanda tarehe 09 Julai 2024, licha ya kuridhishwa na ujenzi wa mradi huo amehimiza wakandarasi kukamilisha kazi kwa wakati ili kwenda sambamba na mkataba.
“Tumekubaliana mwenzi wa tisa lakini mwezi wa kumi nimewapa mimi kwenye mpango inatakiwa mweziw wa tisa mwishoni huu mradi uwe umekamilika,” amesema Dkt Biteko.
Ameweka wazi kuwa serikali imedhamiria kuuingiza Mkoa wa Katavi kwenye historia tangu uhuru kwa mara ya kwanza Mkoa huo kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa.
“Tunaposema umeme wa Gridi ya Taifa maana yake umeme wa uhakika na kutoka kwenye majenereta ambayo yamechoka na ya muda mrefu,” amesisitiza.
Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji TANESCO, Mha. Athanasi Nangali akisoma taarifa ya mradi mbele ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati amesema kuwa kituo cha kupokea, kupoza na kusambaza umeme Mpanda kilianza kujengwa mwenzi Septemba 2021 na sasa kimefikia asilimia 97.
Ameeleza kituo kimeshafungwa transfoma yenye uwezo wamegawati 28 ambapo fedha za ujenzi huo ni bilioni 16.5 za ndani.
Aidha, alibainisha kuwa ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa 132 kutoka Tabora hadi Katavi kwa umbali wa kilomita 383, umefikia asilimia 63 huku matarajio yakiwa hadi kufikia mwezi wa kumi mradi utakuwa umekamilika.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuamua kujenga historia ya kipekee mkoani humo.
Ameeleza kuwa wananchi wanahamu kubwa wa kupatiwa umeme wa Gridi ya Taifa kutokana shughuli za kiuchumi na kijamii kuhitaji umeme.
Mnaweza kushea stori ya Mhe Biteko