TANESCO YAUNGANA NA WAOMBOLEZAJI KATIKA MAZIKO YA WATUMISHI WAKE TANGA WALIOFARIKI KWA AJALI YA GARI

Watumishi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) leo tarehe 17 Septemba 2025 wameungana na familia, ndugu, jamaa na marafiki katika maziko ya watumishi wenzao, marehemu Fransic Kaggi na Elineema Kaggi, pamoja na ndugu zao Janemary Kaggi, Maria Kaggi na Joshua Kaggi.
Maziko ya marehemu hao yamefanyika leo, tarehe 17 Septemba 2025, katika eneo la Kange, Tanga.