
Zoezi la ulipaji fidia kwa wakazi wa Mkata-Handeni na Kilindi mkoani Tanga laanza .Mkuu wa wilaya ya Handeni Mhe. Salum Nyamwese afungua zoezi hilo ambapo kiasi cha shilingi bilioni 1.3 kitalipwa kwa wakazi hao kwa ajili ya kupisha utekelezaji wa mradi wa Gridi Imara katika maeneo yao.