Upepo wa Kimbunga Hidaya umeanza kuleta athari kwenye miundombinu ya umeme hasa baadhi ya maeneo ya ukanda wa Pwani kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara na Pwani. Hali hii inaweza kuleta madhara kwa watu pamoja na mali zao kwenye baadhi ya maeneo. TANESCO inakukumbusha kuchukua tahadhari kwa kutosogelea au kukaa karibu na miundombinu ya umeme. Zingatia tahadhari iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini. Jiweke salama wewe na mali zako. Upatapo changamoto ya huduma, piga 0748550000 kwa msaada zaidi.