loading...

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema tayari mtambo namba nane kutoka kwenye Mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere umekamilika na sasa unaingiza megawati 235 kwenye gridi ya taifa.

Dkt Biteko ametoa taarifa hiyo tarehe 14 Juni 2024 wakati akizindua taarifa za utendaji katika Sekta ndogo ya Umeme, Gesi Asilia na Mafuta kwa mwaka 2022/2023 jijini Dodoma ambapo amesema kwa sasa Jumla ya megawati 470 zinazalishwa kutoka JNHPP na tayari zimeingizwa kwenye gridi ya taifa.